Hafidh Hassan mumewe Rais Samia azikwa Zanzibar

Ibada ya mazishi ya Hafidh iliongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi siku ya Jumatatu saa chache baada ya kufariki kwake.

Tom Mathinji
1 Min Read
Hafidh Ameir Hassan azikwa Zanzibar.

Hafidh Ameir Hassan, mume wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amezikwa katika eneo la Kizimkazi, Kusini mwa jimbo la Unguja, Zanzibar.

Ibada ya mazishi ya Hafidh iliongozwa na Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaabi siku ya Jumatatu saa chache baada ya kufariki kwake.

Viongozi Wakuu serikalini wale wa kisiasa na wa kidini wakiongozwa na makamu wa Rais wa Tanzania Deogratius Ndenjembi,  Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi na Waziri mkuu Mwigulu Nchemba walihudhuria mazishi hayo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Tanzania Deogratius Ndejembi, Hafidh alikuwa akipokea matibabu ya ugonjwa wa moyo na alifariki dunia majira ya saa mbili asubuhi.

Share This Article