Mabingwa mara mbili wa Dunia Ufaransa na Uholanzi walilazimika kutoka tasa katika mechi ya pili ya kundi D kuwania kombe la bara Ulaya, iliyosakatwa ugani Red Bull Ijumaa usiku.
Timu hizo zilidhihirisha mchezo wa haiba kuu lakini zikakosa kumakinika katika safu za mshambulizi.
Nahodha wa Ufaransa Kulian Mbappe alikosa mchuabo huo kutokana na jeraha la pua alilopata katika mchuano dhidi ya Austria.
Kwenye mechi nyingine ya kundi hilo, Austria waliiponda Poland magoli matatu kwa moja.
MGernot Trauner, Christoph Baumgartner na Marko Arnautović walifunga magoli ya Austria dakika za 9, 66 na 78 naye Krzyszto akafunga la kufutia machozi kunako dakika ya 30.
Katika kundi E Ukraine walivuna ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Slovakia.
Ivan Schranz aliiweka Slovakia mbele dakika ya 17 kwa Slovakia,kabla ya Mykola Shaparenko kukomboa kisha Roman Yaremchuk akaongeza la pili dakika ya 80 .
Leo Georgia wataanza na Jamhuri ya Czech saa kumi alasiri, Uturuki wamenyane dhidi ya na Ureno saa moja, kisha Ubelgiji wafunge ratiba dhidi na Romania saa nne usiku.