Chama cha Madaktari nchini (KMPDU) kimetoa ilani ya siku saba kwa serikali kabla ya kuanza mgomo wa kitaifa.
Wakiwahutubia wanahabari leo Jumatatu, maafisa wa chama hicho wakiongozwa na Katibu Mkuu Dkt. Devji Atellah wameishutumu serikali kwa kushindwa kumaliza mgomo wa wauguzi uliodumu kwa zaidi ya siku 40.
Aidha, wamelalama kuwa mgomo huo umesababisha maafa mengi ya wagonjwa wanaokosa huduma katika hospitali za umma na kuapa kusitisha huduma, endapo serikali haitamaliza mgomo wa wauguzi ndani ya wiki moja ijayo.
Dkt. Atellah amesmema imekuwa vigumu na mzigio mkubwa kwa Madaktari kutekeleza majukumu yao katika hospitali za umma kwani wanalazimika kufanya kazi za wauguzi na pia zao kwa wakati mmoja.