Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba, aanguka ghafla

Tukio hilo ilitokea wakati akiendelea kuzungumza. Mzee Warioba alianguka ghafla, hali iliyosababisha shughuli za mkutano kusitishwa kwa muda.

Dismas Otuke
1 Min Read

Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Jaji Joseph Warioba, leo Jumatatu alianguka ghafla wakati akizungumza katika mkutano wa kitaifa wa kutafakari hali ya kisiasa nchini humo.  

Warioba alikuwa akizungumza katika mkutano huo unaoandaliwa na Tanzania Centre for Democracy (TCD), ambapo alizungumzia masuala ya kisiasa na mchakato wa Katiba mpya.

Mwenyekiti wa TCD Dorothy Semu alinukuliwa akisema Jaji Warioba anaendelea vizuri.

Taarifa hiyo inasikitisha ikizingatiwa kuwa Tanzania ingali inaomboleza kifo cha mumwewe Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye alifariki mapema leo Jumatatu.

Share This Article