Simiu na Chebor  ndio mabingwa wa kitaifa wa Mbio za Nyika

Dismas Otuke
1 Min Read

Daniel Ebenyo Simiu na Maurine  Chebor wa  huduma ya kitaifa ya Polisi, ndio mabingwa wa kitaifa wa mbio za nyika zilizoandaliwa katika uwanja wa michezo wa Eldoret siku ya Jumamosi.

Simiu wa idara ya alitetea taji yake katika mbio za kilomita 10 aliyokuwa ameinyakua Februari mwaka huu katuka uwanja uo huo akiziparakasa kwa dakika 30 sekunde 11.1.

Nafasi ya pili ilimwendea Kevin Chesang wa Central Rift kwa dakika 30 na sekunde 12  huku Dennis Kipkoech akiridhia nafasi a tatu.

Chebor ambaye na msimu wa kufana alishinda mbio za wanawake kwa dakika 34 sekunde 16.4 akifuatwa Brenda Jepchumba wa South Rift na  Glorious Jepkirui wa Central Rift waliochukua nafasi za pili na tatu mtawalia.

Cynthia Chepkirui wa  Nairobi  ana Emmanuel wa  North Rift  walishinda bio za kilomita 6 na 8 wasichana na wavulana chini ya umri wa miaka 20 mtawalia.

Wanariadha 30 waiongozwa na bingwa wa Dunia na Olimpiki Beatrice Chebet na mshikilizi wa rekodi ya dunia ya kilomita10 Agnes Jebet Ngetich  Jebet wameteuliwa kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya Mbio za nyika duniani Januari 10 mwaka ujao.

Website |  + posts
Share This Article