Idara ya Uhamiaji yataka shilingi bilioni 4.2 za kuchapisha vitambulisho

Idara hiyo inasema pesa hizo zitasaidia kugharimia takriban vitambulisho milioni sita vinavyokadiriwa kuchapishwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Dismas Otuke
1 Min Read

Idara ya Uhamiaji iliyo chini ya Wizara ya USalama wa Taifa inalitaka Bunge la Kitaifa kuidhinisha bajeti ya shilingi bilioni 4.2 zaidi kugharimia uchapishaji wa vitambulisho vya kitaifa.

Hii inafuatia hatua ya Rais William Ruto kufutilia mbali ada ya shilingi 300 kwa wanaomba vitambulisho kwa mara ya kwanza na pia kusitisha ada nyingine ya shilingi 1,000 kwa wale waliopoteza vitambulisho hadi baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.

Katibu wa Idara ya Uhamiaji na Huduma za Raia Dkt. Belio Kipsang alisema pesa hizo zitasaidia kugharimia takriban vitambulisho milioni sita vinavyokadiriwa kuchapishwa katika kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Dkt. Kipsang alisema hayo alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama wa ndani na uhamiaji.

Aidha, aliongeza kuwa bajeti hiyo mpya itagharimia vitambulisho milioni tatu vipya na vingine milioni tatu kwa waliovipoteza.

Website |  + posts
Share This Article