Gavana wa kaunti ya Machakos Wavinya Ndeti amekana kuhusika katika mizozo inayoshuhudiwa katika Bunge la Kaunti ya Machakos.
Chanzo cha mizozo hiyo ni kuchipuka kwa tofauti kati ya Wawakilishi Wadi juu ya kutimuliwa kwa Spika Anne Kiusya.
Kunao Wawakilishi Wadi wanaounga mkono kutimuliwa kwa Kiusya huku wengine wakipinga vikali.
Pingamizi zilizosababisha vurugu zilizochacha katika ukumbi wa bunge na matokeo yake kuwa kujeruhiwa kwa Wawakilishi Wadi kadhaa wakati wa makabiliano kati yao.
“Sihusiki katika mzozo kati ya Spika wa Bunge la Kaunti ya Machakos na Wawakilishi Wadi,” Gavana Ndeti alibainisha.
“Mara mbili nimemwokoa Spika huyo dhidi ya kubanduliwa madarakani. Siko hapa kulibembeleza bunge hilo. Spika anapaswa kutafuta njia ya kufanya kazi na Wawakilishi Wadi.”