Shughuli ya kuutazama mwili wa Raila yaanza rasmi Kasarani

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto autazama mwili wa hayati Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga.

Shughuli ya umma ya kuutazama mwili wa hayati Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga imeanza rasmi baada ya maafisa wa usalama kurejesha hali ya utulivu katika uwanja wa michezo wa Moi Kasarani Jijini Nairobi.

Rais William Ruto aliongoza viongozi wengine  wa nchi kuutazama mwili huo, kabla ya wananchi kupewa fursa ya kuutazama mwili huo.

Hapo awali, umati mkubwa uliofika katika uwanja huo, ulizua rabsha na kutatiza zoezi hilo na kuwasababisha maafisa wa usalama kutumia vitoa machozi kurejesha hali ya utulivu.

Rabsha hizo zilizuia utaratibu uliokuwa umepangwa awali baada ya kubadilishwa kwa eneo la kuutazama mwili huo.

Maafisa wa usalama wamefaulu kurejesha hali ya kawaida, na kuweka mikakati mwafaka ya kufanikisha shughuli ya umma ya kuutazama mwili wa Odinga.

Kulingana na mipangilio iliyokuwepo awali, shughuli ya kuutazama mwili wa Raila, ilitarajiwa kukamilika saa kumi na moja jioni, na kisha mwili huo upelekwe katika makafani ya Lee.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article