Kiongozi wa chama cha ODM marehemu Raila Odinga alikuwa na ragba kubwa ya michezo sio tu hapa nchini bali pia kimataifa.
Mashindano ya mwisho kwa marehemu Baba kuhudhuria ilikuwa michuano ya kombe la CHAN katika uwanja wa Kasarani kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

Baba alihudhuria takriban mechi zote za timu ya taifa Harambee Stars katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.
Mara ya mwisho alikuwa uwanjani kwenye fainali ya kombe la CHAN kati ya Morocco na Madagascar Agosti 30, wakiandamana na Rais William Ruto, Rais wa shirikisho la soka Afrika CAF Patrice Motsepa
na Rais wa FIFA Gianni Infantino.

Pia alihudhuria na kukutana na wachezaji wa Harambee Stars wakati wa fainali za CHAN.
Baba pia alihudhuria kutazwa kwa klabu ya Police FC kuwa mabingwa wa ligi kuu Kenya kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Ulinzi Complex.

Raila hangekosa uwanjani kila mara Gor Mahia na AFC Leopards walipochuana katika derby ya mashemeji.
Mechi nyingine ambayo hangekosa kuhudhuria ilikuwa ni kati ya Shabana FC na Gor Mahia.

Tukisalia katika soka, marehemu baba amekuwa mlezi wa klabu ya Gor Mahia kuonyesha ari yake michezoni.

Mashindano mengine aliyopenda sana kuhudhuria hayati BABA ni mashindano ya riadha ya Kip Keino Classic Continental Tour yaliyokuwa yakiandaliwa aidha uwanjani Kasarani au Nyayo.
Alihudhuria mashindano hayo akiwa na Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, na pia Rais aliye mamlakani William Ruto.

Mara kwa mara pia Raila alionekana uwanjani kwa mashindano ya humu nchini na pia ya kimataifa.

Baba akiwa Waziri Mkuu katika serikali ya hayati marehemu Rais Mwai Kibaki walipokea Kombe la Dunia mwaka 2009, kabla ya fainali za mwaka 2010.
Kibaki alilibeba kombe hilo huku Raila alipojaribu kuliguza akazuiwa kwani sheria ya FIFA ni kuwa ni Rais pekee anayeruhusiwa kulibeba kombe hilo la kifahari, hali iliyozua mhemko.

Mara kwa mara Baba pia alikuwa akihudhuria mashindano ya kimataifa ya Magical Kenya Open katika uwanja wa Gofu wa Muthaiga.

Baba pia alihudhuria mashindano ya magari ya WRC Safari Rally mjini Naivasha, ambayo yalirejeshwa katika kalenda ya mashindano ya msururu wa magari duniani hapa nchini mwaka 2021 baada ya kuondolewa kwa miaka 19 iliyopita.
Raila Wakaindamana and Rais Ruto alikuhudhuria mashindano ya Odi Genowa katika uwanja wa Homabay mwaka 2024 pamoja na mashindano ya Kip Keino Classic wakiwa na Rais Ruto.

Aidha, Raila alikuwa shabiki wa klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya Uingereza.
Kifupi, Baba Raila alikuwa na mapenzi makubwa kwa michezo, na hangekosa kuhudhuria mashindano ya michezo, na kifo chake ni pigo kubwa kwa tasnia ya michezo nchini Kenya.

Mola ailaze roho ya hayati marehemu Raila Amollo Odinga mahala pema penye wema.

