Shughuli ya kuutazama mwili wa kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga iliyokuwa ianze saa sita adhuhuri katika majengo ya bunge imehamishiwa katika uwanja wa kimataifa Kasarani.
Hii ni kutokana na umati mkubwa wa Wakenya uliojitokeza katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta kuulaki mwili wa Raila.
Aidha, mpango ya kuupeleka mwili wa Baba katika makafani ya Lee pia imefutiliwa mbali.
Wafuasi wa Baba, hadi kufikia saa saba Adhuhuri, walikuwa wangali katika Barabara ya Mombasa kuelekea Kasarani, hali inyohofiwa kuchelewesha zaidi utazamaji wa mwili.
Raila alifariki dunia nchini India mapema Jumatano akipokea matibabu nchini India.