Serikali yatoa hatimiliki 1,283 za ardhi kwa wakazi wa Tana River

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Ardhi Alice Wahome awakabidhi wakazi wa Tana River hati za kumiliki ardhi.

Ni afueni kwa wakazi wa Tana River baada ya serikali ya taifa kuwakabidhi hati 1,283 za ardhi, hii ikiwa ni hatua kubwa kwa mpango wa makazi wa Kipini wa ekari 7,000.

Akitoa hatimiliki hizo, Waziri wa Ardhi, Ujenzi, Nyumba na Maendeleo ya miji Alice Wahome, alitoa wito kwa wakazi hao kuthamini stakabadhi hizo muhimu, na kufanya maamuzi ya busara kuzihusu.

“Unapopata hatimiliki yako, nawahimiza kuwa na majadiliano ya kifamilia, usiwe na haraka ya kuuza ardhi,” alisema Wahome.

Waziri huyo alitoa wito kwa viongozi wa serikali ya taifa na wale wa kaunti, kusaidia katika usajili wa ardhi ya jamii ambayo haijasajiliwa kwa kuwasilisha stakabadhi zinazohitajika.

Kwa upande wake Seneta wa Tana River Danson Mungatana, alipongeza hatua hiyo ya utoaji hatimiliki hizo za ardhi, akisema wamezisubiri kwa muda mrefu.

“Tunafuraha kwamba leo tumepata hatimiliki za ardhi. Tumezisubiri kwa muda mrefu. Tumejitolea kuhakikisha zile ambazo zimesalia zinatolewa,” alisema Mungatana.

Website |  + posts
Share This Article