Serikali kutekeleza operesheni ya kiusalama Laikipia, Meru na Isiolo

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen.

Serikali imetangaza baadhi ya sehemu za kaunti za  Laikipia, Meru, na Isiolo kuwa hatari huku ikilenga kutekeleza operesheni ya kiusalama.

Kwenye Gazeti rasmi la Serikali leo Alhamisi, Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen amesema operesheni hiyo inalenga kutwaa silaha haramu, kuangamiza magenge ya wahalifu huku ikiwapeleka maafisa 400 zaidi wa polisi kufanikisha zoezi hilo.

Baadhi ya maeneo yaliyotajwa kuwa hatari ni pamoja na Laikipia Kaskazini, kaunti ndogo ya Tigania Mashariki, Igembe Kaskazini, na Igembe Kaskazini.

“Tutaimarisha juhudi zetu hadi ujambazi utakapotokomezwa kabisa, na mitandao ya wahalifu kumalizwa,” alisema Murkomen.

Kulingana na Waziri huyo, operesheni hiyo itatekelezwa kwa muda wa siku 30 kuanzia Machi 26,2026.

Sehemu hizo katika siku za hivi karibuni zimeshuhudia wimbi la visa vya uhalifu, ikiwa ni pamoja wizi wa mifugo na ujambazi.

Share This Article