Ruto: Tutawatumikia Wakenya wote kwa usawa

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais William Ruto akiwahutubia wakazi wa Dagoretti Kusini, Nairobi

Rais William Ruto ameahidi kuwa serikali yake itawatumikia Wakenya wote kwa usawa. 

Rais ametoa ahadi hiyo wakati akizindua miradi ya maendeleo katika eneo bunge la Dagoretti Kusini, kaunti ya Nairobi leo Jumatano.

“Tutafanya kazi na kuwatumikia Wakenua wote kwa bidii bila kujali maeneo wanakotoka, dini au kabila,” aliahidi kiongozi wa nchi anayefanya ziara ya wiki moja kwa lengo la kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika kaunti ya Nairobi.

 

Wakati akiwa katika eneo bunge la Dagoretti Kusini, Ruto alizindua ujenzi wa soko la kisasa la Riruta ambalo ujenzi wake utagharimu shilingi milioni 350.

“Soko hilo litatoa mazingira mwafaka kwa wafanyabiashara wadogowadogo, akiwemo Mama Mboga,” aliongeza Rais Ruto.

Aidha, aliweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Ubora cha Dagoretti Jitume.

Ruto alikuwa ameandamana na Naibu wake Prof. Kithure Kindiki na mbunge wa Dagoretti Kusini John Kiarie miongoni mwa viongozi wengine.

Website |  + posts
Share This Article