Kipyegon na Chebet wavunja rekodi za Dunia

Kipyegon aliweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 48 na sekunde 68,akivunja rekodi yake ya Julai mwaka jana ya dakika 3 sekunde 49.04.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon na Beatrice Chebet, walidhihirisha umahiri wao walipovunja rekodi za dunia katika mbio za mita 1500, na mita 5000, katika mashindano ya Diamond League ya Prefontaine Classic jana usiku nchini Marekani.

Kipyegon aliweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 48 na sekunde 68,akivunja rekodi yake ya Julai mwaka jana ya dakika 3 sekunde 49.04.

Deribe Welteji wa Ethiopia alichukua nafasi ya pili huku Jessica Hull wa Australia akiridhia nafasi ya tatu.

 

Chebet aliye katika ubora wake aliweka rekodi mpya ya mita 5000,ya dakika 13 sekunde 58.6,akivunja rekodi ya mwaka 2023 ya Gudaf Tsegay wa Ethiopia ya dakika 14 na nukta 21.

Agnes Jebet Ngetich alimaliza wa pili kwa dakika 14 sekunde 1.29 ,ilihali Tsegay akaambulia nambari tatu.

 

 

Website |  + posts
Share This Article