TSC yamtafuta CEO mpya kumrithi Nancy Macharia anayeng’atuka

Bi Macharia, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza tume hiyo tangu ibuniwe, amekuwa usukani tangu mwaka 2015.

Dismas Otuke
1 Min Read

Tume ya kuwaajiri walimu TSC, imeanza mchakato wa kumtafuta afisa mkuu mtendaji mpya atakayemrithi Nancy Macharia, ambaye muda wake wa kuhudumu unakaribia kukamilika.

Bi Macharia, ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kuongoza tume hiyo tangu ibuniwe, amekuwa usukani tangu mwaka 2015.

TSC iweka tangazo rasmi la uteuzi wa mrithi wa Macharia na kuwataka waliohitimu kutuma maombi.

Afisa mkuu mtendaji wa TSC huwa na ahudumu kwa kipindi cha miaka mitano kinachoongezwa mara moja.

Website |  + posts
Share This Article