Rais William Ruto leo Jumatatu jioni ataondoka nchini kuelekea jijini Doha, Qatar.
Wakati wa ziara yake, Ruto anatarajiwa kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili na wakati huohuo kuvutia uwekezaji.
Aidha, atahudhuria Mkutano wa Pili wa Umoja wa Mataifa, UN Juu ya Ustawi wa Jamii (WSSD2) ambao utaangazia uangamizaji umaskini, kazi nzuri na ujumuishaji katika jamii.
“Akiwa nchini Qatar, Rais Ruto will atahitimisha makubaliano ya uwekezaji muhimu ili kuifanya miundombinu ya Kenya kuwa ya kisasa na kuendeleza miradi muhimu ya nishati na uchukuzi,” ilisema taarifa iliyotumwa na msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed.
“Atafanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa dunia akiwemo His Highness Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani, Sheikh wa Qatar, ili kuimarisha ushirikliano katika biashara, uwekezaji, na mipango ya maendeleo ya kimkakati.”
Rais Ruto akilenga kutumia ziara hiyo kuendeleza uwekezaji uliopanuliwa na ushirikiano wa kimkakati na Qatar katika kilimo, hasa usalama wa chakula, nishati mbadala, afya, utalii na uchukuzi.
Pia atafanya mashauriano na viongozi wa biashara wa Qatar kwa lengo la kupanua ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi.
					
			