Rais William Ruto anatarajiwa kufanya ziara ya siku tano nchini China kati ya Aprili 22 na 26, baada ya kupokea mwaliko wa Rais wa China Xi Jinping.
Ziara ya Ruto inatarajiwa kuangazia kuimarisha uhusiano wa kibiashara baina ya Kenya na China ,ufufuzi wa miradi iliyokwama na kubaini sekta mpya za ushirikiano.
Aidha ziara hiyo inajiri wakati China inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa Marekani iliyoongeza ushuru maradufu kwa bidhaa za China zinazoingizwa Marekani.