KUPPET yataka Hazina Kuu kuwasilisha makato ya bima ya matibabu

Dismas Otuke
1 Min Read
Mgomo wa walimu wa KUPPET wasimamiswa na mahakama.

Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo, KUPPET, kimeitaka Hazina Kuu kuwasilisha makato ya bima ya afya kwa wanachama wake mara moja ili kuwawezesha walimu kupata huduma za matibabu.

Akiwahutubia wanahabari leo jijini Nairobi, kaimu Katibu Mkuu wa KUPPET Moses Nthurima amesema inasikitisha sana kuona kuwa licha ya kuafikiana na serikali mwezi Septemba mwaka jana, wakati wa kusitisha mgomo wa kitaifa, pesa hizo hazijawasilishwa kwa bima ya matibabu ya walimu hadi leo, miezi sita baadaye.

Nthurima amesema hatua hiyo ni ukiukaji wa haki za walimu na  imewafanya wakose huduma bora za matibabu na kushusha motisha na utendakazi.

KUPPET imeitaka Hazina Kuu kuwasilisha hela hizo mara moja ili kuwezesha walimu kupata huduma za matibabu la sivyo huenda wakalemaza huduma.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *