Mshukiwa mmoja wa mauaji ya mwanamuziki wa mtindo wa Rap Pope Smoke amekiri kumuua na kuafikia mapatano ya kifungo cha miaka 29.
Haya janajiri miaka mitano tangu mwanamuziki huyo ambaye jina lake halisi ni Bashar Jackson alipouawa katika eneo la Hidden Hills huko California.
Corey Walker wa umri wa miaka 24 alikiri mashtaka ya mauaji, uvamizi wa makazi na wizi katika mahakama ya Los Angeles Jumatano Februari 5, 2025.
Walker sasa atahudumia kifungo hicho cha miaka 29 gerezani kwa kosa la wizi wa kuvamia nyumba ya mwendazake akiwa na bunduki.
Alikubali pia kwamba alimwibia mwanamke ambaye hajulikani aliyekuwa na Smoke wakati aliuawa.
Jopo la waamuzi lilikuwa likijiandaa kuketi kuamua kesi hiyo iwapo ingeendelea hadi wiki ijayo. Hukumu dhidi ya Walker itasomwa rasmi na jaji katika kikao cha Februari 21, 2025.
Duru zinaashiria kwamba Walker alimpa mtoto bunduki kabla ya kutekeleza uvamizi na wizi hatua ambayo iliishia katika mauaji ya mwanamuziki huyo kwenye nyumba ya kukodisha huko California.
Alikiri pia kuuza saa aina ya Rolex aliyomwibia Pope Smoke kwa dola elfu mbili.
Siku ya tukio, Februari 19, 2020, Walker ambaye alikuwa ameandamana na watoto watatu alivamia nyumba ambayo Pop Smoke alikuwa amekomboa.
Wanadaiwa kufahamu alikokuwa mwanamuziki huyo baada yake kuchapisha mitandaoni picha ya zawadi aliyokuwa amepokea na anwani ikawa inaonekana kwenye picha hiyo.
Smoke ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 20, alikuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap na mmoja wa waanzilishi wa kundi la Brooklyn drill movement.