Mtangazaji wa Pwani Fm Eric Mgenge maarufu kama Gates Mgenge alishinda tuzo ya mtangazaji bora wa redio kwa upande wa wanaume kwenye tuzo za African Golden.
Aliwapiku wakenya wenzake Willy M. Tuva, Alex Mwakideu, Maina Kageni, Watanzania Lil Ommy, Millard Ayo, Watangazaji wa Afrika Kusini Robert Marawa, Africa Melane, Sol Phenduka, Thato Sikwane kati ya wengine wengi.
Tuzo za African Golden ziliandaliwa Mei 3, 2025 katika hoteli ya Emara Ole-Sereni jijini Nairobi nchini Kenya.
Kulingana na waandalizi, hafla ya kutoa tuzo kwa washindi ilikuwa pia mkusanyiko wa wataalamu wa sekta mbali mbali, jukwaa la kusherehekea ufanisi na fursa ya kuonyesha talanta zinazotambulisha Afrika katika jukwaa la ulimwengu.