Mwanamuziki na mwigizaji wa Marekani Olurotimi Akinosho maarufu kama Rotimi amefichua kwamba mwanamuziki Jay Z alimsaidia pakubwa kunoa makali ya uigizaji.
Rotimi alikuwa kwenye kundi moja la waimbaji kwa jina NBH ambapo wanachama wengine walikuwa wapwa wa mwanamuziki nguli Jay Z.
Wanachama wa NBH walikuwa wakiandika nyimbo na kuziimba nyumbani ambapo Jay Z alikuwa anahudhuria mikutano yao ya mazoezi ili kuwakosoa.
Rotimi anasema Jay alitambua talanta yake mapema na akawa anamfundisha jinsi ya kuimba jukwani kana kwamba yeye ni mtu mzima na mwanamuziki ambaye amebobea.
Mafundisho hayo ya Jay Z yalimsaidia Rotimi kuboreka katika uigizaji na anasema kama sio yeye hangekuwa alipo sasa.
Rotimi aliigiza kama Dre kwenye filamu ya “Power” ya mwanamuziki 50 Cent na baadaye akaingilia mtindo wa muziki wa Nigeria afrobeat.
wazazi wa Rotimi ni wa asili ya Nigeria.
Usaidizi wa Jay Z unaendelea kumsaidia hadi sasa kwani alimaliza kuigiza kwenye awamu ya 7 ya kipindi “The Chi” Oktoba 9, 2024.
Ameigiza kwenye ‘Boss’ kama mlanguzi wa dawa za kulevya, akaigiza kwenye vipindi vitatu vya ‘Betray’ kwenye ABC, filamu ya ‘Black Nativity’ ya mwaka 2013 kati ya nyingine nyingi.
Muziki wake pia umechezwa kwenye majukwaa mbali mbali huku akiimba jukwaani kwenye matamasha ya wanamuziki kama Jennifer Hudson, T.I., Estelle na NERD.