Mwanamuziki wa Tanzania Juma Mussa Mkambala maarufu kama Juma Jux alifunga ndoa na mpenzi wake wa asili ya Nigeria Priscilla Ojo.
Hafla hiyo ilifanyika Ijumaa Februari 7, 2025 na ilikuwa ya kiisilamu ambapo Priscilla ambaye alikuwa mkristo alibadili dini na kuwa muisilamu.
Binti huyo wa mwigizaji wa Nigeria Iyabo Ojo alipatiwa jina jipya la dini ya kiisilamu ambalo ni Hadiza Mkambala.
Priscilla ambaye hujihusisha na masuala ya mitindo ya mavazi alipendeza sana wakati wa harusi yake ambapo alivaa vazi la rangi ya dhahabu huku mamake mzazi akichagua vazi la rangi ya kahawia.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu kadhaa maarufu nchini Tanzania wakiwemo Diamond Platnumz na Zuchu, huku wengine kama Nandy wakiamua kupongeza wanandoa hao kwenye mitandao ya kijamii.
Iyabo Ojo alichapisha picha za hafla hiyo kwenye akaunti yake ya Instagram akisema kwamba hafla hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza katika ndoa ya binti yake na Juma Jux na zimesalia nyingine nne.
“Mungu tunakupa utukufu wote. Moja imeisha bado nyingine 4. Pongezi wanandoa Mkambala.” aliandika mama huyo wa watoto wawili.