Mwigizaji na mwimbaji wa Uingereza Cynthia Chinasaokwu Onyedinmanasu Amarachukwu Owezuke Echimino Erivo maarufu kama Cynthia Erivo kwa mara nyingineamezungumzia kuhusu kukataliwa na babake mzazi.
Alikuwa akihojiwa na jarida moja ambapo alisema babake alimkataa yeye na dadake, wakati huo akiwa na umri wa miaka 16 pekee.
Erivo ambaye umaarufu wake umeongezeka kwa kiwango kikubwa katika miaka ya hivi karibuni anashangaa jinzi maisha yake yangekuwa, iwapo babake angekuwepo hadi sasa.
Lakini tena alisema kwamba hataki hata kuwazia hilo kwani anajua babake hatarejea kwenye maisha yake na kwamba anafurahia maisha yake yalivyo sasa.
Mwaka 2021 ndio erivo alizungumzia tukio hilo kwenye mahojiano na jarida jingine ambapo alisema wakati huo alikuwa amekaa miaka 10 bila kumtia mzee huyo machoni. Mara ya mwisho walionana ni katika harusi ya binamu yake.
Erivo anasema babake aliwataarifu kuhusu kukatiza uhusiano naye na dadake mdogo wakiwa katika kituo cha treni na mamake akachukua majukumu yote ya kuwalea huko London.
Familia hiyo ilihamia Uingereza miaka ya awali kukwepa vita nchini Nigeria.
Wakati wa maadhimisho ya siku ya kina baba duniani, Cynthia alilalamika kuhusu matukio mengi ya maisha yake ambayo babake amekosa na mengi atayoendelea kukosa huku akishukuru kina baba walio kwenye maisha yake.
