Rais Suluhu ala kiapo baada ya kushinda uchaguzi mkuu

Kenya iliwakilishwa na Naibu Rais Kithure Kindiki katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa mataifa ya kigeni, mabalozi na viongozi wakuu serikalini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameapishwa kwa muhula mwingine siku ya Jumatatu baada ya kushinda uchaguzi mkuu kwa kupata asilimia 98 ya kura zilizopigwa wiki jana.

Suluhu ameapishwa katika uwanja wa Kijeshi mjini Dodoma spamoja na Makamu wake Emmanuel Nchimbi.

Hafla ya uapisho imehudhuriwa na viongozi kadhaa wa mataifa ya kigeni, mabalozi na viongozi wakuu serikalini.

Kenya iliwakilishwa na Naibu Rais Kithure Kindiki.

Akihutubu baada ya kula kiapo, Suluhu amesema atahakikisha usalama unadumishwa na kulinda mali.

Aidha, amewapongeza wapinzani wake 16 waliotoa ushindani hafifu kabisa katika uchaguzi  huo mkuu.

Uchaguzi wa Tanzania ulikumbwa na utata huku watu kadhaa wakiripotiwa kuuawa katika hatua ambayo iliibua shutuma za kimataifa.

Wakosoaji wa uchaguzi huo wanasema Suluhu aliwakandamiza wapinzani wake wakuu ili asikumbane na ushindani mkali kwenye uchaguzi huo ambao aliibuka mshindi kwa asilimia 98 ya kura zilizopigwa.

 

Website |  + posts
Share This Article