Rais William Ruto amesema serikali imestawisha na kuimarisha sekta ya sukari nchini chini ya utawala wake wa miaka minne.
Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Wanahabari katika kaunti ya Kisumu, Ruto amesema kuna usimamizi mpya katika viwanda vyote vya serikali vya kusaga miwa.
Aliongezea kuwa kinyume na awali wakulima wanaowasilisha miwa hulipwa kila wiki huku wanaocheleshwa sana wakipokea malipo yao ndani ya mwezi mmoja.
Rais ameongeza pia kuwa wafanyakazi ambao walikuwa wakicheleweshwa mishahara kwa sasa wanalipwa kwa wakati ufaao kila mwezi.
Amesema kuwa kwa sasa kuna viwanda vitano vipya vilivyosajiliwa maajuzi huku vingine vitatu vikitarajiwa kufunguliwa.
Ruto amesema kuwa serikali itatenga ekari 300 za ukuzaji miwa huku nchini hii ikitarajiwa kuanza kuuza sukari nje ya nchi .