Rais Ruto: Kilimo kimenawiri ndani ya miaka minne

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto amesema mpango wa serikali yake wa kupunguza bei ya pembejeo za kilimo umezaa matunda, huku mavuno ya wakulima yakiongezeka.

Akizungumza kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Wanahabari katika Ikulu ndogo ya Kisumu Jumatatu usiku, Rais Ruto alisema kuna jumla ya Wakulima milioni 7.3 waliosajiliwa na ambao hupokea mbolea iliyopunguzwa bei.

Rais alisema ilikuwa hiari yake kupunguza bei ya mbolea kutoka shilingi elfu tano hadi elfu mbili kwa sasa, huku pia bei ya mbegu ikipunguzwa ili kuongeza uzalishaji.

Aidha, Rais alisema usajili wa wakulima umeiwezesha serikali kutoa mbolea ya ruzuku kulingana na kiwango cha shamba la kila mkulima.

Ruto alisema uzalishaji mahindi nchini umeongezeka kutoka magunia milioni 44 hadi 75  kwa mwaka huku pia uzalishaji wa kahawa,sukari na chai ukiongezeka.

Share This Article