Mwamuzi wa Slovenia, Slavko Vinčić,atakuwa msimamizi wa fainali ya Kombe la Dunia kati ya Uhispania na Mabingwa watetezi Argentina leo Jumapili, katika uwanja wa Metlife mjini New York.
Refarii huyo atasaidiwa na Tomaž Klančnik na Andraž Kovačič,wote kutoka Slovenia, huku Adham Makhadmeh wa Jordan akiwa afisaa wa nne.
Itakuwa mechi ya nne kwa mwamuzi huyo kusimamia katika kipute cha mwaka huu baada ya kuwa Pilato wa mchuano wa kundi C, kati ya Brazil na Morocco,ule kati ya Jordan na Algeria, na mechi ya awamu ya 32, baina ya Mexico na Ecuador.
Aidha,Vinčić alikuwa refarii wa kwanza kutoa kadi nyekundu kwa beki wa Ecuador Piero Hincapié, baada ya kumwongelesha mchezaji wa Mexico akiwa amefumba mdomo.