Idara ya mahakama nchini Uganda yaanza kuskiza rufaa za uchaguzi mkuu

Majaji 100 wamejukumiwa kuskiza kesi 346 za rufaa za uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama nchini Uganda mapema Jumatatu imeanza kuskiza kesi za rufaa za kupinga matokeo ya viti mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa mapema mwaka huu.

Majaji 100 wamejukumiwa kuskiza kesi 346 za rufaa za uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Majaji 48 wa Mahakama Kuu na Mahakimu 52 wataskiza kesi 30 zilizowasilishwa katika Mahakama mbalimbali nchini humo.

Kesi hizo zinatokana na uchaguzi wa mabara ya miji na Ubunge baina ya Septemba 14 na Novemba 13 mwaka huu.

Majaji wa Mahakama Kuu wataskiza jumla ya kesi 157 huku Mahakimu wakitengewa kesi 189.

Share This Article