Rais Ruto: Wakenya zaidi watapata ajira nchini Qatar

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto na waziri wa leba wa Qatar Ali Bin Samikh Al-Marri, katika Ikulu ya Nairobi.

Rais William Ruto amesema kuwa Wakenya zaidi watapat fursa ya kufanya kazi nchini Qatar, punde tu mkataba wa maelewano kati ya nchi hizo mbili utaanza kutekelezwa mwezi Disemba mwaka 2024.

Akizungumza alipokutana na waziri wa leba wa Qatar Dkt. Ali Bin Samikh Al-Marri  katika Ikulu ya Nairobi Jumatatu, kiongozi wa taifa alisema Wakenya sasa wafanya kazi katika sekta za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ICT, Elimu na Hoteli, na watapokea malipo sawa na wenzao wa kimataifa.

“Kenya na Qatar zinaimarisha ushirikiano wao. Tunajizatiti kuondoa vikwazo vya usafiri wa kikazi, ili kutoa nafasi za ajira kwa raia walio na utaalam wa Kenya na Qatar,” alisema Rais Ruto.

Alipongeza Qatar kwa kufungua kituo cha Visa Jijini Nairobi, akiongeza kuwa hatua hii itarahisisha mchakato wa kupata hati za kusafiria kwa wakenya wanaopanga kufanya kazi katika nchi hiyo.

Rais Ruto alisema mazungumzo yao pia, yaliangazia uwekezaji wa Qatar hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kupiga jeki mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.

Kwa upande wake, waziri Al-Marri alipongeza ushirikiano baina ya Kenya na Qatar akisema taifa lake lina sekta zinazohitaji wakenya walio na ujuzi.

Share This Article