Zaidi ya watu 200 wafariki kwenye ajali ya ndege India

Tom Mathinji and BBC
1 Min Read
Ndege ya India yaanguka na kuwaua watu zaidi ya 200.

Ndege ya shirika la ndege la India iliyokuwa na zaidi ya watu 200, imeanguka muda mfupi baada ya kuanza safari kutoka uwanja wa ndege wa Ahmedabad magharibi mwa India, maafisa wanasema.

Faiz Ahmed Kidwai, Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka ya usafiri wa anga ya India, aliambia shirika la habari la Associated Press kwamba Ndege ya Air India AI171, ilianguka katika eneo la makazi linalofahamika ka Meghani Nagar dakika tano baada ya kuanza safari mwendo wa saa saba na dakika thalathini na nane 1:38pm (08:08 GMT) siku ya Alhamisi.

Alisema kuwa abiria 232 na wafanyakazi 12 walikuwa ndani ya ndege hiyo iliyokuwa ikielekea uwanja wa ndege wa London Gatwick nchini Uingereza.

Ndege hiyo imeanguka katika eneo la makaazi, karibu na uwanja wa ndege wa Ahmedabad – polisi wanasema ilianguka katika maazi ya madaktari hali ambayo umelemaza shughuli ya uokoaji.

Picha zilizosambazwa mitandaoni zinaonyesha moshi ukifuka kutoka eneo la ajali karibu na uwanja wa ndege wa jiji hilo.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article