Siwezi kumwacha baba nikae na Mbosso – Baba Levo

Baba Levo amesema hayo leo alipokuwa akiondoka Tanzania kwenda kujiunga na Diamond Platnumz Uingereza.

Marion Bosire
1 Min Read

Mtangazaji wa Wasafi Fm Clayton Revocatus Chipando maarufu kama Baba Levo ambaye pia ni mshawishi mkubwa mitandaoni nchini Tanzania leo ameondoka nchini humo kuelekea London kuungana na Diamond Platnumz.

Akizungumza na wanahabari katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere muda mfupi kabla ya kuondoka, Baba Levo alielezea kwamba alikuwa amealikwa na Mbosso kwa shughuli ya leo ila hangeweza kuhudhuria.

Baba Levo ambaye hujiita Chawa wa Diamond ambaye anamrejelea kama baba alisema hawezi kumwacha babake akakae na mtoto akimaanisha Mbosso.

Mbosso kwa sasa anaendeleza hafla ya kusikilizwa kwa nyimbo zake mpya kwenye EP yake aliyoipa jina la Room Number 3 – RN3 katika ukumbi wa Mlimani City jioni ya leo.

Diamond Platnumz aliondoka Tanzania jana akiwa ameandamana na mwanamuziki mwenza Juma Jux kwa ajili ya tamasha lake la kesho Ijumaa Juni 13, 2023 katika ukumbi wa Royal Albert jijini London.

Baada ya London, Diamond anatarajiwa kuzuru Manchester kabla ya kuelekea nchini Marekani kwa tamasha la Summer Jam Ijumaa Juni 20, 2025 katika ukumbi wa Prudential center.

Baba Levo alisema atakuwa na Diamond katika ziara hiyo huku akijisifia kwamba ni yeye pekee aliyepatiwa Visa ya Uingereza kati ya machawa wote nchini Tanzania.

Website |  + posts
Share This Article