Wachimba migodi wawili wafariki Kakamega

Tom Mathinji, Radio Taifa and Radio Taifa
1 Min Read

Wachimba migodi wawili wa umri wa makamo wameripotiwa kufariki baada ya kuta za mgodi walimokuwa wakichimba kuporomika na kuwaangukia katika eneo la Ikolomani, kaunti ya Kakamega. 

Waathiriwa walifariki baada ya kukosa hewa ya kutosha.

Aliyeshuhudia kisa hicho alisema mmoja wa waathiriwa ambaye alikuwa anasimamia  kazi hiyo, aliingia kwenye mgodi kukagua shimo baada ya kiwango cha maji kupungua.

Alipokosa kurejea haraka, mwathiriwa wa pili naye aliingia mgodini ili kumsaka mwenzake. Patrick Misango, ambaye ni mchimbaji migodi, ametoa wito kwa serikali kuwapa vifaa bora vya kuchimba migodi na kuboresha mikakati ya usalama.

Mwenyekiti wa wachimbaji migodi katika maeneo ya Shinyalu na Ikolomani, Samwel Njomo, alilalamikia  ukosefu wa msaada wa serikali.

Mama wa mmoja wa waathiriwa alisikitika kupokea habari hizo za kutamausha.

Miili ya waathiriwa hao wawili imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Kakamega.

TAGGED:
Share This Article