Hakuna tishio la uchaguzi mkuu, asema Rais Suluhu

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Samia Suluhu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayewania muhula wa kwanza ofisini, ametoa hakikisho kuwa uchaguzi mkuu wa wiki ijayo utaendelea kama ilivyoratibiwa.

Akipiga kampeni za dakika za mwisho mapema wiki hii, Rais Samia amesema hakuna tishio lolote litakalozuia uchaguzi kufanyika.

Uchaguzi mkuu wa Tanzania utaandaliwa Oktoba 29 mwaka huu huku Rais Suluhu akiwania muhula wake wa kwanza ofisini.

Hii ni baada ya kukamilisha muhula wa pili wa hayati Rais John Pombe Magufuli aliyefariki punde tu baada ya kuchaguliwa kwa muhula wa pili.

Hata hivyo, Suluhu anakabiliwa na upinzani hafifu huku kiongozi wa upinzani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, Tundu Lissu, akisalia korokoroni kujibu kesi ya uhaini.

Pia mpinzani mwingine, Luhana Mpina wa chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT), alifungiwa nje ya kinyang’anyiro cha Ikulu na tume ya uchaguzi nchini humo.

Website |  + posts
Share This Article