Waziri wa zamani wa Leba Florence Bore ni miongoni mwa watu wengine 11 walioteuliwa kuiwakilisha Kenya kama Mabalozi katika nchi mbalimbali nchini.
Bore, aliyetimuliwa serikalini kufuatia mabadiliko ya Baraza la Mawaziri, ameteuliwa kuhudumu kama Balozi wa Kenya nchini Namibia.
Galma Mukhe Boru ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya mjini Addis Ababa, Ethiopia wakati Anthony Mwaniki Muchiri akiteuliwa kuhudumu kama Balozi wa Kenya nchini Uturuki.
Wengine walioteuliwa kuhudumu kama Mabalozi ni Lucy Kiruthu (Thailand), Henry Wambuma (Burundi), Catherine Kirumba Karemu (Tanzania), George Morara Orina (Ireland na Abdirashid Salat Abdille (Indonesia).
Kwa upande mwingine, Maurice Odhiambo Makolo ameteuliwa kuhudumu kama Balozi wa Kenya nchini Uingereza, Joseph Musyoka Masila (Saudi Arabia), na Edwin Afande (Austria).
Majina yao yamewasilishwa kwa Bunge la Taifa ili kupigiwa msasa na kuidhinishwa kabla ya uteuzi wao rasmi.
Wengine walioteuliwa na Rais Ruto ni wakuu wa balozi ndogo za Kenya na Manaibu Mabalozi.
