Raila awaomba wanahabari msamaha baada ya kushambuliwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Kiongozi wa muungano wa Azimio  Raila Odinga amewaomba msamaha wanahabari walioshambuliwa na wahuni siku ya Jumatano katika afisi za Wakfu wa Jaramogi Oginga Odinga.

Katika taarifa kwa wanahabari mapema leo Alhamisi, Raila amesikitishwa kuwa wanahabari waliokuwa wakifuatilia kikao cha Azimio walishambuliwa na kundi la vijana wahuni, akiahidi kufanywa kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha uvamizi huo uliovuruga mkutano wao.

Aidha, amewaomba radhi viongozi wengine wa muungano huo waliovamiwa akiahidi kuchukuliwa kwa hatua kali kwa waliohusika na uvamizi huo.

Vijana hao watundu walivuruga kikao cha wanahabari kilichokuwa kikihutubiwa na kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka, aliyepinga ofa ya Rais William Ruto katika kubuniwa kwa Baraza jipya la Mawaziri.

Vijana hao takriban 50 walivamia kikao hicho na kuamrisha kila mtu kuondoka huku wakirusha viti na kuwajeruhi waliokuwepo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *