Polisi wanamtafuta mshukiwa wa wizi Marsabit

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mshukiwa huyo alijisingizia kuwa mteja, akitaka asafirishwe hadi katika eneo la Majengo.

Tom Mathinji
1 Min Read
Polisi wanamtafuta mshukiwa wa wizi Marsabit.

Maafisa wa Polisi wameanzisha uchunguzi kumsaka mshukiwa wa wizi aliyetoroka baada ya kumuibia mwendashaji wa pikipiki katika kaunti ya Marsabit.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mshukiwa huyo alijisingizia kuwa mteja, akitaka asafirishwe hadi katika eneo la Majengo.

Walipofika katika eneo hilo la Majengo, mshukiwa huyo alitoa bastola na kumuibia mfanyabiashara huyo pikipiki yake yenye nambari za usajili KMGV 939W.

Wakati wa makabiliano hayo, mshukiwa huyo aliangusha bastola aina ya Ceska, kabla ya kutoroka na pikipiki.

Bastola hiyo pamoja na risasi zilichukiwa na polisi na sasa zinazuiliwa katika kituo cha polisi cha Marsabiti, zikisaidia kwenye uchunguzi.

Polisi wanafuatilia vyanzo muhimu kumkamata mshukiwa huyo pamoja na kupata pikipiki iliyoibwa.

TAGGED:
Share This Article