Omdurman wadumisha rekodi ya asilimia 100 katika Ligi ya Mabingwa Afrika

Dismas Otuke
2 Min Read

Al Hilal Omdurman ya Sudan ndiyo timu pekee iliyodumisha rekodi ya asilimia 100, baada ya michuano ya mzunguko wa pili hatua ya makundi kuwania taji la ligi ya Mabingwa Afrika.

Al Hilal wakiwa nyumbani waliizabua TP Mazembe kutoka jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo mabao 2-1 katika kundi A huku MC Alger ya Algeria pia ikisajili ushindi wa 2-0 dhidi ya Young Africans.

Hilal wanaongoza kundi hilo kwa alama 6 wakifuatwa na Alger kwa pointi 4, huku Mazembe wakizoa alama moja pekee nao Young Africans hawana pointi baada ya mechi mbili.

Kundini B, FAR Rabat ya Morocco ilitoka sare ya goli moja na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wakati Maniena ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo ikilazimishwa sare ya goli moja nyumbani dhidi ya Raja Casablanca.

Rabat wanaongoza kwa alama nne katika kundi hilo,wakifuatwa na Sundowns na Maniema kwa alama 2 kila moja, huku Casablanca wakiwa na pointi moja.

Mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri walitoka sare tasa katika kundi C dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini nao stade d’ Abidjan kutola Ivory Coast ikipigwa laza bao moja kwa bila na CR Belouizdad kutoka Algeria.

Ahly maarufu kama Red Devils wanaongoza kundi hilo kwa pamoja na Pirates kwa pointi nne kila moja ,moja zaidi ya Belouizdad huku Abidjan ikishika nanga pasi na alama.
Group C

Djoliba ya Mali waliambulia sare tasa dhidi ya Pyramids ya Misri katika kundi D nao Sagrada Esperança ya Angola na Esperance Tunis wakitoka sare kappa katika kundi D.

Esperance na Pyramids wanaongoza kundi hilo kwa alama 4 kila moja, wakifuatwa na Sagrada Esperança na Djoliba ya Mali kwa alama moja kila moja.

Kipute hicho kitarejea Disemba 13 na 14 kwa mechi za mzunguko wa tatu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *