Mwili wa Gatwiri kuzikwa Ijumaa ijayo

Marion Bosire
1 Min Read

Familia ya mwigizaji na muunda maudhui mitandaoni Brenda Tabitha Gatwiri imetangaza kwamba mwili wake utazikwa nyumbani kwa babake huko Meru, Ijumaa Novemba 15, 2024.

Hafla ya mazishi kulingana na tangazo hilo itakuwa kituo cha utamaduni cha Thiiri kwenye barabara kuu ya kutoka Meru kuelekea Ruiri kuelekea Isiolo, karibu na soko la Mugene.

Baada ya mkutano na ibada ya mazishi, mwili wa Gatwiri utazikwa nyumbani kwa baba yake, umbali wa kilomita kama moja hivi kutoka eneo la mkutano.

Familia ya mwendazake pia inaomba msaada wa kifedha wa kumpa hafla faafu ya mwisho ulimwenguni, na michango inaweza kutumwa kwenye nambari ya “Paybill” ambayo ni 891300 nambari ya akaunti ikiwa 106473.

Mwili wa Gatwiri uligunduliwa kwenye nyumba yake ya kupangisha yapata wiki moja iliyopita na kakake ambaye aliamua kumzuru baada yake kukosa kujibu jumbe zake na hata kukosa kuchukua simu.

Uchunguzi wa maiti yake uliofanyika katika makafani ya hospitali ya chuo kikuu cha Kenyatta ulibaini kwamba aliaga dunia kwa kushindwa kupumua ipasavyo kutokana na namna alikuwa amelala.

Share This Article