Murkomen atoa onyo kali kwa maafisa wa usalama wafisadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Murkomen awaonya maafisa wa serikali wafisadi.

Waziri wa Usalama wa Taifa Kipchumba Murkomen, ametoa onyo kali kwa maafisa wa usalama wanaoshiriki ufisadi, akisema watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Waziri huyo aliwaonya maafisa wa serikali ya taifa, maafisa wa huduma ya taifa ya polisi na maafisa wa polisi wa akiba wanaojihusisha na ufisadi kwamba watakapo kamatwa wataona cha mtema kuni.

“Ufisadi hudumaza juhudi za serikali za kuwahudumia wananchi.  Mteja wetu mkuu ni mwananchi wa Kenya,” alisema Murkomen.

Alidokeza kuwa visa kama vile ulanguzi wa binadamu na utozaji wananchi ada za kupata vitambulisho, havitavumiliwa kamwe na serikali.

“Machifu, Manaibu wa Chifu na Manaibu wa kamishna wa kaunti watakaopatikana wakijihusisha na ufisadi hawatasazwa. Hakuna kosa ndogo kuliko lingine,” aliongeza waziri huyo.

Murkomen alisisitiza kuwa utoaji huduma kikamilifu kwa wananchi, ni muhimu kuhakikisha kuwa utawala wa Rais Ruto unatimiza ahadi zake.

Website |  + posts
Share This Article