Maafisa wa upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) wamemkamata mshukiwa wa wizi wa kimabavu na kupata bastola moja katika eneo la Likoni kaunti ya Mombasa.
Kulingana na maafisa hao wa DCI, bastola hiyo inaaminika kuwa imetumiwa kutekeleza visa kadhaa vya uhalifu.
Mshukiwa huyo Paul Odhimabo mwenye umri wa miaka 27, alikamatwa baada ya kutekelezwa operesheni ya polisi katika hoteli moja lililoko eneo la Mariakani.
Bastola hiyo aina ya CZ, iliyokuwa imefichwa mvunguni mwa kitanda, imekabidhiwa maabara ya kitaifa kwa uchunguzi wa kisayansi.