Magari yateketea kwenye shindano la mbio za magari Botswana

Marion Bosire
1 Min Read

Magari yapatayo 49 yaliteketea katika mji wa Jwaneng nchini Botswana Jumapili, Juni 25, 2023 ambapo wamiliki walikuwa wamefika kushuhudia shindano la uendeshaji magari jangwani.

Ajali hiyo inasemekana kutokea saa saba unusu mchana wenyewe wakiwa mbali kidogo na eneo la maegesho ya magari kushabikia shindano hilo kwa jina “Toyota Desert Race-2023”.

Hakuna kifo kilichoripotiwa kutokana na ajali hiyo.

Wamiliki wa magari hayo walipigwa na butwaa waliporejea katika eneo hilo na kupata magari yao yakiwa yamechomeka huku mengine yakiendelea kuchomeka.

Maafisa wa polisi wanachunguza chanzo cha moto huo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *