Mkutano wa pili wa tume ya kudumu ya Mozambique na Uganda waanza jijini Kampala

Marion Bosire
1 Min Read

Mkutano wa pili wa tume ya pamoja ya kudumu ya Uganda na Mozambique umeanza leo katika hoteli ya Mestil jijini Kampala nchini Uganda. Mkutano huo utaangazia usalama, utalii, mawasiliano pamoja na uchimbaji madini.

Uganda na Mozambique zimefurahia uhusiano mwema tangu awali hatua iliyosababisha kubuniwa kwa tume ya pamoja ya kudumu mwaka 1987.

Mkutano wa kwanza wa tume hiyo uliandaliwa jijini Maputo nchini Mozambique mwaka 1988.

Mwaka 2028 nchi hizo mbili ziliafikia makubaliano kuhusu nyanja za ushirikiano kwa lengo la kuboresha hata zaidi uhusiano kati yazo, makubaliano yaliyotiwa saini jijini maputo mwaka huo wa 2018.

Wajumbe wa mkutano huo wataangazia pia utekelezaji wa maelekezo ya Rais yaliyotolewa wakati Rais wa Mozambique Filipe Jacinto Nyusi alizuru Uganda Aprili 2022.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo, balozi Richard Kabonero mkuu wa ushirikiano wa kikanda wa kiuchumi katika wizara ya masuala ya kigeni nchini Uganda aliwakaribisha wajumbe wa mkutano huo.

Kabonero alisema anatumai kwamba mkutano huo utafanikisha uhusiano imara wa kibiashara na uwekezaji kati ya Uganda na Mozambique.

Share This Article