Misri na Mali watinga nusu fainali ya AFCON U 23

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa watetezi Misri na Mali walijikatia tiketi ya nusu fainali ya makala ya tatu ya kuwania kombe la bara Afrika kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 23 nchini Morocco, Jumamosi usiku baada ya kusajili ushindi wa pili kila moja.

Misri waliibwaga Gabon magoli mawili kwa nunge katika mechi iliyosakatwa ugani Ibn-Batouta mjini Tangier.

Mahmoud Hassan na Osama Abdelhady, walipachika goli moja kila mmoja katika dakika za mwisho mwisho za mechi na kuwapa Pharoes ushindi uliowahikishia uongozi wa kundi A na kuweka miadi ya kukabiliana na Guinea katika nusu fainali .

Mamadou Sangare wa  Mali akisherehekea kupachika  bao katika mechi dhidi  Gabon katika uwanja  Tangier Grand Stadium ©Nour Akanja/BackpagePix

Mali almaarufu The Flying Eagles pia walifuzu kwa nusu fainali baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Niger, katika mechi nyingine ya kuhitimisha ratiba ya kundi B ugani Prince Moulay Abdellah Sports Complex mjini Rabat na kumaliza ya pili kwa alama 6.

Mali watachuana na wenyeji Morocco katika semi fainali ya Jumanne.

Fainali ya mashindano hayo itaandaliwa Julai 8 katika uwanja wa Prince Mouley Abdellah jijini Rabat huku timu tatu bora, zikifuzu kwa michezo ya olimpiki mwaka ujao nchini Ufaransa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *