Pyramids FC walinyakua kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza, baada ya kuwalemea Mamelodi Sundowns 2-1 kutoka Afrika Kusini, uwanjani 30 June jijini Cairo Jumapili usiku.
Wenyeji walichukua uongpozi kunao dakika ya 23 kupitia kwa Fiston Mayele, kabla ya beki Ahmed Samy, kuongeza la pili kipindi cha pili.
Iqraam Rayners alikomboa moja dakika ya 75 kwa wageni .
Pyramids waliibuka washindi wa jumla kwa mabao 3-2 na kuwa timu ya nne ya Misri, kunyakua kombe hilo baada ya Al Ahly,Zamalek na Ismaily.