Mili 18 yatolewa katika majengo yaliyoangushwa na jeshi la Israel

Dismas Otuke
1 Min Read

Wafanyikazi kwa kukabiliana na dharura wameondoa mili 18, kutoka kwa vifusi vya nyumba mbili  zilizobomolewa na majeshi ya Israel, katika eneo la Khan Younis kusini mwa ukanda wa Gaza kwa mjibu wa shirika la habari nchini Palestina WAFA.

Mili hiyo ilijumuisha watoto tisa, na wanawake wawili .

Haya yanajiri huku makabiliano kati ya jeshi la Israel na wanamgambo wa Hamas nchini Palestina, yakiingia siku ya sita katika ukanda wa Gaza mapema Alhamisi.

Wizara ya afya nchini Palestina imetangaza kuwa idadi ya vifo kutokana na mashambulizi hayo imefikia 1,2000 huku majeruhi wakifikia 5,600 .

Upande wa Israel waliofariki wamefikia 1,200 na wengine 3,000 wakijeruhiwa.

Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa Wapalestina 338,934, wamepoteza makazi kufuatia mashambulizi hayo katika ukanda wa Gaza ambao hali yake imedorora zaidi kutokana na ukosefu wa nguvu za umeme,chakula na maji.

Share This Article