Ndege yaanguka ikiwa na abiria 12 Kwale

Tom Mathinji
1 Min Read
Watu 12 wafariki kwenye ajali ya ndege Kwale.

Ndege iliyokuwa na abiria 12, imeanguka Jumanne asubuhi katika kaunti ya Kwale.

Halmashauri ya Kusimamia Safari za Ndege Nchini (KCAA) kwenye taarifa fupi Jumanne asubuhi, imesema kuwa ndege hiyo yenye nambari za usajili 5y-CCA, ilikuwa ikisafiri kutoka Diani kuelekea Kichwa Tembo ajali hiyo ilipotokea.

Kulingana na Halmashauri hiyo, ndege hiyo ilianguka mwendo wa saa kumi na moja asubuhi.

“Asasi za serikali tayari zimefika kwenye eneo la ajali kubainisha chanzo cha ajali hiyo na athari zake,” ilisema KCAA kupitia kwa taarifa.

Tutakuletea habari zaidi kuhusu ajali hiyo punde tunapozipokea….

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article