Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara amechaguliwa kwa muhula wa nne kwa ushindi mkubwa katika uchaguzi wa marudio, kulingana na matokeo ya muda yaliyotangazwa Jumatatu, matokeo ambayo yalitarajiwa kwa kiasi kikubwa baada ya wapinzani wake wakuu kuonekana kutokuwa na ushawishi.
Alassane Ouattara mwenye umri wa miaka 83 alipata asilimia 89.77% ya kura zilizopigwa.
Mtangulizi wake, Laurent Gbagbo, alikataa kukiri kushindwa katika kinyang’anyiro kilichopita, na kusababisha vita vya miezi minne vilivyoua takriban watu 3,000.
Waziri wa zamani wa Biashara Jean-Louis Billon, ambaye alikubali kushindwa na Ouattara siku ya Jumapili, alipata asilimia 3.09% ya kura, huku mke wa rais wa zamani Simone Gbagbo akipata asilimia 2.42%, kulingana na matokeo yaliotolewa kwenye televisheni ya serikali na Ibrahime Coulibaly-Kuibiert, rais wa tume ya uchaguzi.
Simone Gbagbo alimpigia simu Ouattara siku ya Jumatatu kumpongeza kwa ushindi wake, chanzo kiliiambia Reuters.