MCK yakashifu ukandamizaji wa wanahabari

Tom Mathinji
1 Min Read
MCK yalaani ukandamizaji wa wanahabari.

Baraza la Vyombo vya habari humu nchini MCK, limekashifu vikali kukamatwa na kushambuliwa kwa wanahabari, waliokuwa wakiripoti matukio ya maandamano siku ya Jumanne katikati mwa Jiji la Nairobi.

Maandamano hayo yaliandaliwa, kupinga Mswada wa fedha wa mwaka 2024.

Kupitia kwa taarifa, baraza hilo lilisema limesikitishwa kwamba wanahabari ambao walitarajia usalama wa maafisa wa polisi wakiwa kazini, walishambuliwa, kudhulumiwa na kutiwa nguvuni na maafisa wa polisi hata baada ya wao kujitambulisha kwa maafisa hao.

“Hatua hiyo ilijiri hata baada ya wanahabari kutambuliwa na kadi za MCK na mavazi ya wanahabri,” ilisema taarifa.

Takriban wanahabari watano, wawili kutoka mashirika ya kimataifa ya vyombo vya habari, na watatu wa Kenya, walikamatwa wakiwa wanatakeleza majukumu yao.

Afisa huyo,mkuu mtendaji wa MCK, alimtaka Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome, kuwachukulia hatua maafisa hao na kuhakikisha kuwa wanahabari wanalindwa na si kulengwa kwa kunyanyaswa, wanapotekeleza majukumu yao.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *