Mbunge wa Malava Moses Malulu Injendi ameaga dunia leo akipokea matibabu katika hospitali ya Aga Khan kaunti ya Nairobi.
Kifo cha Mbunge huyo kimethibitishwa na Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula.
Hadi kifo chake, Malulu alikuwa mbunge wa Malava na pia Naibu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge kuhusu Elimu na Utafiti.
Marehemu amehudumu bungeni tangu mwaka 2013.
Miongoni mwa waliomwomboleza ni Wetang’ula, kiongozi wa wengi Kimani Ichung’wah, Mbunge wa Saboti Caleb Amisi, na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika chama cha ODM Philip Etale.