Mbivu na mbichi kubainika kundi A mechi za AFCON U 23

Dismas Otuke
1 Min Read

Kipute cha kuwania kombe la AFCON kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 23, kitaingia mechi za raundi ya pili hatua ya makundi leo Jumanne usiku ambapo Guinea watafungua ratiba dhidi ya Congo saa mbili usiku katika uwanja wa Prince Mouley Abdellah  jijini Rabat.

Baadaye saa tano usiku, wenyeji Morocco watapambana na Ghana katika kiwara kicho hicho.

Guinea na Congo watachuana kila timu ikihitaji ushindi ili kusalia mashindanoni, baada ya timu zote kupoteza mechi za ufunguzi.

Mshindi wa mchuano huo atakuwa na fursa ya kufuzu kwa semi fainali huku atakayepoteza akiyaaga mashindano.

Katika mechi ya pili Morocco na Ghana, watakuwa wakisaka ushindi wa pili huku mshindi akifuzu kwa nusu fainali.

Timu  zote zilipata ushindi katika mechi  za ufunguzi Ghana ikiishinda Congo nao Morocco wakailemea Guinea.

Mashindano hayo yatakamilika Julai 8 na  yanatumika kuchagua timu tatu zitakzowakilisha Afrika kwa michezo ya Olimpiki mwaka 2024 jijini Paris, Ufaransa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *